Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO inarahisisha tiba na huduma kwa wagonjwa wa akili

WHO inarahisisha tiba na huduma kwa wagonjwa wa akili

Shirika la afya duniani WHO leo limetoa muongozo ambao utawasaidia mamilioni ya watu duniani wenye maradhi yasiyotibika kama ya akili, msongo wa mawazo, mishipa ya fahamu na athari za matumizi ya mihadarati na ulevi wa kupindukia.

Muongozo huo utasaidia kukabiliana na matatizo ya msongo wa mawazo, maradhi yatokanayo na ulevi wa kupindukia, kifafa na matatizo mengine ya akili yanayojulikana katika vituo vya afya. Umuhimu wa muongozo huo ni kurahisisha utoaji wa huduma kwa waathirika kwenye vituo vya afya kama anavyofafanua mkurugenzi mkuu wa WHO Bi Margareth Chan kuwa tatizo ni kubwa.

(SAUTI YA MARGARETH CHAN)

Ameongeza kuwa leo hii tunapiga hatua kubwa kushughulikia matatizo hayo, hasa idadi ya wagonjwa nay a wale wanaopata tiba, kwani katika baadhi ya nchi pengo ni kubwa sana hadi asilimia 80, ni mzigo mkubwa na hauwezi kupuuzwa.