Skip to main content

Baada ya mafanikio ya mkutano wa malengo ya milenia Ban agusia mambo muhimu kwa miezi ijayo

Baada ya mafanikio ya mkutano wa malengo ya milenia Ban agusia mambo muhimu kwa miezi ijayo

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon kwa mara nyingine ameitaka Israel kusitisha ujenzi wa makazi ya walowezi katika eneo la Wapalestina linalokaliwa Ukingo wa Magharibi.

Katika mkutano wa kila mwezi na waandishi wa habari unaohusu masuala mbalimbali leo Jumatano Ban ametoa wito wa kupigwa hatua za majadiliano baina ya Israel na Palestina. Amesema katika siku za hivi karibuni amezungumza na wahusika wakuu kutoka kila upande ikiwa ni pamoja na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na kiongozi wa Palestina Mahmoud abbas.

(SAUTI YA  BAN KI-MOON)

Katika mkutano huo pia Ban amesisitiza uhusru wa mahaka inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa kubaini ukweli wa mauaji ya waziri mkuu wa zamani wa Lebanon Rafiq Hariri na wengine 22 mwaka 2005. Pia amekanusha madai kwamba ripoti ya hivi karibuni ya Umoja wa Mataifa kuhusu mauaji ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imepunguzwa makali ili wkuwastahi nchi jirani na Congo zilizoshutumiwa kwenye ripoti hiyo ambao pia wanachangia vikosi vya kulinda amani.

Kuhusu kura ya maoni ya Sudan Kusini Katibu Mkuu ameonya kwamba endapo haitashughulikiwa ipasavyo inaweza kuzusha tafrani kubwa na kurejesha machafuko nchini humo.  Amesema kura hiyo ikifanyika vyema itasaidia kujenga hatma na kuimarisha maisha ya mamilioni ya watu wa taifa hilo. Kura ya maoni Sudan Kusini ni hatua ya mwisho katika mkataba wa amani wa 2005 CPA uliomaliza miongo miwili ya vita biana ya Sudan Kaskazini na Kusini.