Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mamia wafa na maelfu hatarini kwa athari za madini Nigeria

Mamia wafa na maelfu hatarini kwa athari za madini Nigeria

Athari za kimazingira kutokana na madini ya risasi katika jimbo la Zamfara nchini Nigeria zimesababisha vifo vya mamia ya watu hadi sasa huku maisha ya maelfu ya wengine yakiwa hatarini.

Kundi la wataalamu watano kutoka shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP na kutoka kwa ofisi ya kuratibu masaula ya kibinadamu OCHA wanasema kuwa hatua za haraka zinahitajika.

Magonjwa yanayo sababishwa na sumu ya madini ya risasi na vifo vilianza kuripotiwa mapema mwaka huu kwenye wilaya mbili za mkoa wa Zamfara baada ya hatua za wenyeji za kuchimba dhahabu kutoka kwa udongo ulio na madini ya risasi nje na ndani ya nyumba zao wakati wataalamu hao wanasema kuwa vifo vingi vimetokea bila kuripotiwa.

Kundi hilo la wataalamu pia linasema kuwa utafiti zaidi unahitaja kwa vyakula kama nyama na kuongeza kuwa athari zaidi zinatoka maeneo ya kutayarishia madini hayo na kutoa wito wa kutumika ka njia mwafaka kwa mfano shughuli ya kusafishwa kwa madini kuendeshwa mbali na vijiji wanamoishi watu.