Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM kuorodhesha njia 30 kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa

UM kuorodhesha njia 30 kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa

Shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP linatarajiwa kutoa ripoti ya uchunguzi kila siku kwa muda wa siku 30 zijazo ili kuthibitisha kuwa suluhu katika kukabilina na mabadiliko ya hali ya hewa zikiwemo za upanzi wa miti na matumizi ya nguvu za jua vinapatikanana.

Ripoti hiyo inayofahamika kama "njia 30 kwa siku 30" ilizindulia nchini Mexico kwenye mkutano ulioandaliwa na UNEP na mashirika mengine ya kimataifa. Katibu mkuu wa shirika la UNEP Achim Steiner anasema kuwa kwa sasa suala muhimu ni kuangazia mabadiliko kwa ulimwengu wote.

Imebainika kuwa ili kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa nchi matajiri zitahitajika kupunguza gesi inayochafua mazingira kwa kati ya asilimia 25 na 40 itimiapo mwaka 2020 na kupunguzwa hadi nusu ifikapo mwaka 2050.

Hata hivyo utafiti wa kwanza wa UNEP utahusu utoaji wa mikopo kwa nishati ya jua baada ya mpango kama huo wa shirika la UNEP nchini India kwa ushirikiano na mabenki mawili makuu nchini humo kuwapa mikopo ya faida ndogo watu ili kuwazesha kununua vifaa vinavyotumia nishati ya jua mwaka 2003.