Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCAP yazindua kundi kuchagiza uwezeshaji kwa wanawake

UNESCAP yazindua kundi kuchagiza uwezeshaji kwa wanawake

Ikiwa ni miaka 10 tangu kupitishwa azimio namba 1325 kwenye baraza la kuhusu wanawake, amani na usalama, Dr Noeleen Heyzer mkuu wa tume ya Umoja wa Mataifa ya masuala ya uchumi na jamii kwa ajili ya Asia na Pacific ESCAP amezindua kundi la kikanda kutoa ushauri wa masuala ya uwezeshaji wa wanawake.

Kundi hilo litatoa ushauri kwa serikali, jumuiya za kijamii na wadau wengine kuahakikisha azimio 1325 linatekelezwa katika kanda ya Asia-Pacific. Kundi hilo la ushauri linajumuisha wanawake na wanaume wenye uzoefu unaojulikana katika kuchagiza ushiriki wa wanawake kwenye mchakato wa amani na usalama .

Miongoni mwa watu hao ni Amartya Sen mshini wa tuzo la amani la nobel ambaye atakuwa mshauri mkuu wa kundi hilo, Bi Sima Samar ambaye ni mkuu wa tume huru ya haki za binadamu Afghanistan na Bi Teresita Quinto-deles mshauri wa Rais wa masuala ya amani nchini Ufilipino. Bo Heyzer amesema amani itakayopatikana kwa kuwashirikisha wanawake ni kwa faida ya jamii nzima.

(SAUTI YA NOELEEN HEYZER)