Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi 22 zakabiliwa na changamoto kubwa ya njaa:FAO

Nchi 22 zakabiliwa na changamoto kubwa ya njaa:FAO

Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO limesema nchi 22 duniani zinakabiliwa na changamoto kubwa kama matatizo ya chakula na njaa yanyojirudia kutokana na mchanganyiko wa majanga ya asili, vita na uongozi mbaya.

Haya yamejitokeza katika ripoti ya FAO ya hali ya usalama wa chakula duniani 2010 iliyochapishwa leo kwa ushirikiano na shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa WFP. Jason Nyakundi anayo maelezo zaidi.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

Kupitia kwa ripoti ya mwaka huu kuhusu hali ya chakula duniani iliyotolewa ba shirika la chakula na kilimo duniani FAO na lile na mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa  WFP ni kuwa idadi ya watu wanaokabiliwa na ukosefu wa chakula duniani kwenye nchi hizi na mara tatu zaidi kuliko walio kwenye nchi zinazoendelea.

Ripoti hiyo pia inaonyesha kuwa watu milioni 166 wanakubwa na ukosefu wa lishe kwenye nchi zinazokabiliwa na na majanga ya mara kwa mara kote duniani . Hata hivyo kiasi kikubwa cha misaada kinachopelekwa katika nchi hizi sana sana vyakula husaidia katika uwekezaji wa siku zijazo kwa nchi hizo na kuonyesha vile misaada ya vykula inaweza kuwa suluhu la muda mrefu.

Shirika la FAO linasema kuwa watu 925 kote duniani wanakabiliwa na hali mbaya ya njaa baada ya idadi hiyo kupungua kutoka watu bilioni 1.020 mwaka uliopita.