Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kukamatwa kamanda wa Mai Mai DRC ni muhimu:UM

Kukamatwa kamanda wa Mai Mai DRC ni muhimu:UM

Umoja wa Mataifa umekaribisha hatua ya kukamatwa luteni kanali Mayele wa kundi la Mai Mai Cheka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Mayele anadaiwa kuandaa na kuongoza ubakaji wa watu wengi wanawake, wanaume na watoto katika eneo la Walikale nchi Congo hivi karibuni.

Mwakilishi maalumu wa Katibu mkuu kwa masuala ya watoto kwenye vita vya kutumia silaha Radhika Coomaraswamy amesema hatua hiyo iliyofanywa na mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo MONUSCO imekuja wakati muafaka kwani ubakaji ni kosa la jinai lilsilovumilika.

Naye mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu katika masuala ya ukatili wa kimapenzi katika vita Margot Wallstrom amesema kukamatwa kwa kamanda huyo ni ushindi hasa kwa maelfu ya wanawake walioathirika na ubakaji. George Njogopa na taarifa zaidi.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

Margot Wallstron amepongeza hatua ya kukamatwa kiongozi wa waasi anayetuhumiwa kuhusika katika kisa cha ubakaji wa zaidi ya wanawake 300, kaskazini mwa nchi hiyo Margot Wallstron ambaye anauzuru eneo hilo amesema kuwa kukamatwa kwa kiongozi huyo ni habari njema kwa watu wa nchi hiyo na ni ushindi katika masuala ya haki, hususan kwa wanawake ambao walikumbwa na vitendo hvyo vya ubakaji na unyanyasaji mwingine wa kijinsia na kwamba sheria itachukua mkondo wake.

Margot Wallstron ameeleza kuwa kamanda wa kundi hilo la waasi wa Mai Mai Cheka, aliyejulikana kama Luteni Kanali Mayele alikamatwa katika operesheni iliyofanywa kikosi cha Umoja wa Mataifa cha kulinda amani kwa kushirikiana na majeshi ya serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.