Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Senegal kuwasaidia watoto walioathirika na usafirishaji haramu wa watu

Senegal kuwasaidia watoto walioathirika na usafirishaji haramu wa watu

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM linapanga kutoa mafunzo ya siku tatu kwa washirika wake nchini Senegal ambao wapo mstari wa mbele katika kukabiliana na usafirishaji bianadamu hasa zaidi watoto.

Mafunzo hayo yanalenga kutekeleza mradi maalumu unaojulikana kama ufungua mpya kwa watoto waliochukuliwa na kupelekwa sehemu za mbali kwa ajili ya kutumikishwa katika kazi. IOM imechukua jukumu hilo kama sehemu yake ya kukabiliana na wimbi la biashara ya usafirishaji binadamu katika eneo la Afrika Magharibi.

Eneo la afrika magharibi linatajwa kuwa kinara wa biashara ya kusafirisha watoto ambao husafilishwa kwenye maeneo mbalimbali kwa ajili ya kutumikishwa katika kazi. Inadariwa kwamba kila mwaka kati ya watoto 200,000 hadi 300,000 husafirishwa.

Mafunzo hayo ambayo yanaanza Dakar Octoba 6,yanataka kutoa mwanga namna ya kuwasaidia watoto waliosafirishwa kurejea kwenye maisha ya jamii ya kawaida na kuboresha mashirikiano zaidi baina ya mashirika ya kiraia na taasisi za kiserikali jinsi ya kuwalinda watoto hao.