Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yaanzisha mtandao kuwaunganisha Wazambia ughaibuni

IOM yaanzisha mtandao kuwaunganisha Wazambia ughaibuni

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM kwa ushirikiano na idara inayoshughulikia masuala ya raia wa Zambia walio mataifa ya kigeni, Zambia sasa inalenga kufanya utafiti na kukusanya maoni ya raia wake wake walio nje walio na nia ya kuwekeza nchini mwao kwa manufaa ya taifa hilo.

Utafiti huo pia unatarajiwa kuonyesha waliko raia hao wa Zambia , mali yao , wangepenfda kufanya nini pamoja na ujuzi wa kazi walio nao. Mkuu wa IOM Andrew Choga anasema kuwa utafiti huo utafungua mawasilino mapya yatakayochangia kuwepo kwa ushirikiano na maendeo .

Anasema kuwa raia wa zambia walio mataifa ya kigeni mara nyingi huuliza maswali kuhusu uraia na sheria zinazoambata na uwekezaji. Mpango huu utaisaida serikali kuwafikiksha habari raia wake wanaoshi mataifa ya kigeni na kuwazesha kuchangia kwenye maendeleo ya kitaifa na kuhakikisha wamepata habari wa urahisi na pia kuondoa vizingiti vinavyowazuia kuwekeza nyumbani