Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi wa Burundi walioko DRC warejea nyumbani

Wakimbizi wa Burundi walioko DRC warejea nyumbani

Mamia ya wakimbizi wa Burundi wamevuka mpaka kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na kurejea nyumbani.

Wakimbizi hao walikwenda Congo zaidi ya muongo uliopita na hatua ya kurudi nyumbani shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linasema ni mwanzo wa hatua ya kurejea kwa hiyari kwa wakimbizi hao.

Wakimbizi hao ambao 240 wamesafirishwa asubuhi ya leo ni miongoni mwa wakimbizi 10,000 wanaotarajiwa kurudi nyumbani Burundi katika miezi michache ijayo, na kila wiki kutakuwa na kundi la wakimbizi watakaosafirishwa amesema Adrian Edward msemaji wa UNHCR

(SAUTI YA ADRIAN EDWARD)

Ameongeza kuwa wengi ya wakimbizi hao wanapowasili nyumbani wanaweza kushiriki kwenye mpango wa UNHCR wa kuwarejesha wakimbizi katika maisha ya kawaida mpango unaowagawia huduma za afya, elimu na malazi.

Kuna jumla ya wakimbizi 165,000 wa Burundi DRC na karibu 80,000 katika nchi jirani na Burundi. Kwa zaidi ya miezi sita iliyopita zaidi ya nusu wamerejea kwa hiyari , Burundi pia inahifadhi wakimbizi 41,000 wa Congo na mpango huu wa pande mbili wa kurejea kwa hiyari ni matokeo ya makubaliano kati ya UNHCR, Burundi na DRC