Skip to main content

Timor-Leste imepiga hatua katika haki za binadamu:UM

Timor-Leste imepiga hatua katika haki za binadamu:UM

Ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu nchini Timor-Leste iliyotolewa leo mjini Dili inasema nchi hiyo imepiga hatua katika haki za binadamu ikiwemo kuimarisha usalama, mifumo ya sheria na kufanyia marekebisho baadhi ya sheria.

Ripoti hiyo ya UNMIT ambayo hutolewa kila mwaka imezingatia kipindi cha kuanzia Julai 2009 hadi Juni mwaka 2010 pia imeelezea kuendelea kuwepo kwa matatizo ya haki za binadamu ikiwa ni pamoja na ukiukaji unaofanywa na vikosi vya usalama, ukosefu wa haki kwa washutumiwa na changamoto za kukabiliana na ukiukaji uliofanywa miaka ya nyuma.

Hata hivyo ipoti hiyo imesema kuna matumaini hasa baada ya hatua nzuri kupigwa katika jeshi la polisi la nchi hiyo na wizara ya sheria. Kumetolewa mafunzo maalumu kwa wafanyakazi wa idara hizo, kuboreshwa kwa huduma vijijini na kupitishwa kwa sheria dhidi ya ukatili majumbani.