Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pakistan bado inakabiliwa na matatizo:UNHCR

Pakistan bado inakabiliwa na matatizo:UNHCR

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linasema ingawa mafuriko ya Pakistan hayagongi tena vichwa vya habari kimataifa, lakini nchi hiyo bado inakabiliwa na matatizo makubwa.

Shirika hilo linasema mamilioni ya watu bado wanahitaji msaada na katika jimbo la Sindh mafuriko yanaendelea na theluthi mbili ya watu milioni 30.4 wa jimbo hilo wameathirika huku wengine milioni 1.6 wamepoteza makazi. Jason Nyakundi na taarifa zaidi

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

Majuma kumi na moja tangu kutokea mafuriko ya kwanza nchini Pakistan bado hali ya mamilioni ya waathiriwa wa mafuriko hayo inatajwa kuwa mbaya. Bado mafuriko yanaendelea kuripotiwa katika mkoa wa Sindh ulio kusini ambao karibu watu milioni 1.6 hawaka makao. Nalo ziwa manchar ambalo ni ziwa kubwa zaidi lisilokuwa na chumvi limevurika na kupasua kingo zake kwa muda wa majuma mawili yaliyopita na kusababisha watu zaidi kuhama makwao.

Kwa sasa shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limetoa misaada kwa watu 192,800 katika mkoa wa Sindh yakiwemo mahema na vifaa vingine. UNHCR kwa upande mwingine inashughulikia wakimbizi milioni 1.7 na wengine milioni 1.1 waliokimbia makwao kutokan na mizozo ambao nao pia wameithirika kutokana na mafuriko hayo.