Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM watoa wito kuwasaidia waliopoteza makazi Kurdistan Iraq

UM watoa wito kuwasaidia waliopoteza makazi Kurdistan Iraq

Mtaalamu wa masuala ya haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa ametoa wito kwa utawala katika eneo la Kurdistan nchini Iraq kuchukua hatua za haraka kuwasaidia takriban watu 30,000 waliopoteza makwao na ambao kwa sasa wanaishi katika hali ya umaskini na kukosa huduma muhimu kama elimu , makao na afya.

Akikamilisha ziara ya juma moja nchini Iraq mwakilishi wa katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki Moon kuhusu haki za wakimbizi wa ndani Walter Kälin ameitaka serikali ya eneo la Kurdistan kuchukua hatua za kuhakikisha kwa usalama wa kutosha na pia kushughulikia masuala ya kiuchumi na ya kijamii ya familia hizo.

Kalin amesema kuwa wale ambao hawana uwezo wa kujitafutia makoa au hawana nia ya kurudi makwao wanastahii kupewa makao au ardhi na kuwakaribisha wale wakimbizi wanaongia sasa hasa kutoka maeneo ya mipaka ya nchi majirani yanayoshambuliwa kwa mabomu.

 Kalin ameongeza kuwa wakimbizi hao wa ndani wako kwenye hatari ya kudhulumiwa akisema wakati akina na watoto wakiwa ndio tegemeo la familia huenda wakaanguka mikononi mwa walanguzi wa binadamu na dhuluma zingine.