Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Misitu na bayo-anuai lazima vilindwe, kwani viko hatarini:FAO

Misitu na bayo-anuai lazima vilindwe, kwani viko hatarini:FAO

Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO limesema bayo-anuai ya misitu ya dunia iko hatarini kutokana na ongezeko la ukataji miti, mmomonyoko wa ardhi na kupungua kwa maeneo ya kupanda miti.

FAO inasema hata hivyo katika nchi nyingi juhudi zinaendelea na kutoa matumaini kwa kuwa na maeneo ya hifadhi ya misitu na bayo-anuai. Ripoti ya kimataifa ya kwanza ya aina hiyo kutathimini rasilimali ya misitu FRA 2010 imetolewa leo na FAO mjini Roma katika mwanzo wa mkutano wa kamati ya shirika hilo ya misitu katika wiki ya kimataifa ya misitu.

Katika ripoti hiyo Amerika Kusini imeelezewa kushina nafasi kubwa ya kutoweka kwa misitu ikifuatiwa na Afrika na Asia. Teresa Presas ni Rais wa baraza la kimataifa la misitu, ICFPA.

(SAUTI YA TERESA PRESAS)

Wiki hiyo ya misitu iliyoanza leo itakamilika Oktoba 8 na inatoa fursa ya waliokutana kubadilishana mawazo, taarifa na kuelezea mafanikio waliyoyapata katika uhifadhi wa misitu, na pia nini kifanyike zaidi kuilinda.