Skip to main content

Migogoro inaongeza wimbi la wakimbizi duniani:Guterres

Migogoro inaongeza wimbi la wakimbizi duniani:Guterres

Kamishna mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR Antonio Gurerres leo ameonya kuwa ongezeko la migogoro inayoendelea kwa muda mrefu inasababisha kuwepo na tatizo la kudumu la wakimbizi duniani.

Amesema hali hii inahitaji suluhu na kuangaliwa kwa kina hasa katika kuwalinda watu takribani milioni 43 ambao wamelazimika kuwa wakimbizi wa ndani duniani.

Katika hotuba yake ya ufunguzi wa kamati ya utendaji ya UNHCR bwana Guterres amesema hali ya wakimbizi, wanaoomba hifadhi, wasio na utaifa, wakimbizi wa ndani na wengine wanaohitaji msaada inakuwa ngumu kila mfano, mfano Afghanistan na Somalia. George Njogopa ana maelezo zaidi

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

Amesema nguvu ya pamoja inahitajika sasa ili kuweza kuwanusuru watu zaidi ya milioni 43, walioko mtawanyikoni kutokana na sababu mbalimbali. Akifungua mkutano mkuu wa bodi ya watendaji ExCom,

Guterres ametaja mambo kadhaa ikiwemo kukosekana kwa udhabiti wa makazi, mtawanyiko wa wakimbizi, pamoja na kuongezeka kwa idadi ya watu wanaoomba hifadhi, na kuendelea kukosekana kwa hifadhi maalumu, ni changamoto nyingine ambayo utatuzi wake bado kufikiwa.

Guterres ametolea mfano nchi kama Afghanistan na Somalia, ambazo zimeendelea kuzalisha wakimbizi kutokana na machafuko yanayoibuka mara kwa mara.