Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Leo ni siku ya kimataifa ya wazee, tuwaenzi:Ban

Leo ni siku ya kimataifa ya wazee, tuwaenzi:Ban

Leo ni siku ya kimataifa ya wazee ikiwa ni mwaka wa kumi tangu kuanza kuadhimishwa rasmi kwa siku hiyo.

Katika ujumbe maalumu wa siku hii Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema wazee wana jukumu kubwa katika kila jamii, kama viongozi, watoa huduma na wanaojitolea, lakini ndio watu ambao wanakabiliwa na ubaguzi, kuteswa, kutelekezwa na kufanyikwa ukatili.

Amesema idadi ya wazee inaongezeka haraka na inakadiriwa kuwa ifikapo 2050 kutakuwa na wazee bilioni mbili duniani jambo ambalo litatuathiri wote amesema. Ametoa wito kwa nchi kujitahidi kushughulikia matatizo na mahitaji ya wazee, ikiwemo kuwapa huduma zinazostahili, mipango ya fmafao ya uzeeni na kuweka sheria na sera ambazo zitazuia ubaguzi wa rika na jinsia makazini.

Rozina Chimbalani ni ajuza wa miaka 77 nchini Malawi anasema unapokuwa mzee unakabiliwa na matatizo mengi lakini lazima ujikimu kimaisha.

(SAUTI ROZINA MALAWI)