Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ripoti ya UM kuhusu ukiukaji wa haki za binadamu DR Congo yaishutumu Rwanda na Uganda

Ripoti ya UM kuhusu ukiukaji wa haki za binadamu DR Congo yaishutumu Rwanda na Uganda

Ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyoandaliwa na ofisi ya tume ya haki za binadamu imetoka leo ikielezea ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu uliofanyika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kati ya mwaka 1993 na 2003.

Akizungumza na Radio ya Umoja wa Mataifa mkuu wa haki za binadamu Navi Pillay amesema ripoti hiyo ni ya kukabiliana na ukwepaji wa sheria na kuhakikisha wahusika wanafikishwa kunakostahili kwani mamilioni ya watu wameathirika na uasi huo.

(SAUTI NAVI PILLAY)

Matukio hayo 600 yalichangia pia katika vifo vya idadi kubwa ya raia, ubakaji, matumizi ya watoto katika vita na kusababisha mamilioni kuzikimbia nyumba zao. Ripoti hiyo imezishutumu baadhi ya nchi kuhusika kwa njia moja au nyingine kuchangia matukio hayo Rwanda imeshutumiwa kutekeleza uhalifu wa vita dhidi ya Wahutu walioko Jamhuri ya Kidemokrasia ya congo. Nchi hiyo imekanusha vikali shutma hizo na kutishia kujitoa katika mpango wa kulinda amani.
Uganda nayo imeshutumiwa kwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu madai ambayo yameikasirisha Uganda na kupitia balozi wake kwenye Umoja wa Mataifa Ruhakana Rugunda imesema inaipinga ripoti hiyo.

(SAUTI RUHAKANA RUGUNDA)

Na kuhusu tishio la awali la Uganda kwanba ripoti hiyo ikiyoka itaathiri ushiriki wa mipango ya amani ya kikanda Rugunda amesema

(SAUTI RUHAKANA RUGUNDA)

Nchi nyingine zilizoguswa katika ripoti hiyo ni Burundi, Zimbabwe na Angola. Na waziri wa mambo ya nje ya Angola Georges Chikoti amesema ripoti hiyo haikuzingatia taratibu zinazotakiwa.

(SAUTI GEORGES CHIKOTI)