Skip to main content

ITU na Ureno kutoa msaada wa kompyuta katika nchi zinazoendelea

ITU na Ureno kutoa msaada wa kompyuta katika nchi zinazoendelea

Shirika la Umoja wa Mataifa la mawasiliano ITU na serikali ya Ureno wanashirikiana kutoa kompyuta mpakato au lap top mashuleni katika nchi zinazoendelea.

Katika mradi huo wa pamoja waliouiuta "unganisha shule, unganisha jamii" Ureno kupitia mpango wake wa kimataifa wa uitwao eSchool itasaidia kutoa msaada wa teknolojia kwa shule kwenye nchi mbalimbali. Nchi 20 zitanufaika katika awamu ya kwanza ambazo zitafanya majaribio ya mtazamo wa kutumia taarifa na mawasiliano ya teknolojia (ICT) madarasani na kupima matokeo yake.
Shule moja katika nchi hizo 20 zitapata kompyuta mpakato 50 ambazo ni mpya na zilizo tayari za kifaa cha kufundishia, masuala ya kufundishwa pamoja na broadba iliyounganishwa na internet. Katibu mkuu wa ITU Hamadoun Toure ameipongeza serikali ya Ureno kwa kuwa tayari kutoa uzoefu wake kwa nchi zingine. Mradi huo ulioanza mwaka jana nia yake ni kusaidia wadau wa umma na binafsi kuziunganisha shule zote na huduma ya internet ili ziweze kutumia pia kama vituo vya ICT vya mawasiliano kwa jamii.