Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tatizo la ajira limedhoofisha mtazamo wa nchi nyingi

Tatizo la ajira limedhoofisha mtazamo wa nchi nyingi

Ripoti mpya ya utafiti ya kitengo cha shirika la kazi duniani ILO inasema tatizo la ajira la muda mrefu limedhoofisha mtazamo wa kijamii nchi nyingi.

Ripoti hiyo iitwayo "Ripoti ya kazi duniani 2010 kutoka tatizo moja hadi jingine" inasema baada ya miaka mitatu ya matatizo sasa uchumi wa dunia unaanza kukua tena, huku nchi nyingine zikishuhudia dalili za matumaini ya kutengemaa kwa ajira na hususan katika nchi ambazo uchumi wake unachipukia kama za Asia na amerika ya Kusini.

Hata hivyo ripoti hiyo ya taasisi ya kimataifa ya masomo ya ajira ya ILO imeonya kuwa licha ya hatua hizo nzuri zilizoanza kujitokeza , wingu jingine zito limejitokeza katika sekta ya ajira na katika nchi nchi hali imekuwa mbaya.

(SAUTI KUTOKA ILO)