Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uganda yakasirishwa na ripoti ya UM kuhusu DR Congo

Uganda yakasirishwa na ripoti ya UM kuhusu DR Congo

Serikali ya Uganda imekasirishwa vikali na ripoti ya awali iliyovuja ya Umoja wa Mataifa ambayo inaishutumu nchi hiyo kwa uhalifu wa vita nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Ripoti hiyo ambayo inaelezea vita vya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kati ya mwaka 1993 na 2003 inalishutumu jeshi la Uganda kutekeleza uhaklifu wa vita na uhalifu dhidi ya ubinadamu ilipowasaidia waasi wa Congo walioupindua utawala wa Rais Mobuto Sese Seko mwaka 1997 na kudhibiti sehemu ya mashariki mwa nchi hiyo.