Mataifa zaidi yatia saini mkataba wa kutosajili watoto jeshini

29 Septemba 2010

Mataifa 11 zaidi yamejiunga na mpango wa Umoja wa Mataifa yanayounga mkono kukomeshwa kuajiriwa kwa watoto jeshini, kusadia kuwandoa watoto waliojiunga na makundi ya wapigananji na kuwasaia kurejea kwenye maisha ya kawaida.

Sasa kujiunga kwa mataifa hayo kwenye makubalino kumeongeza idadi ya nchi zinazoyaunga mkono kuto 84 hadi 95 . Mwakilishi maalum wa katibu mkuu wa UM kwenye masuala ya watoto na mizozo Radhika Coomaraswamy amesema kuwa kutumiwa kwa watoto vitani ni kama uhalifu wa kivita.

Amesema kuwa katika juhudi za kulinda watoto wa wa wakati huu na wa siku sijazo ni lazima ihakikishwe kuwa wanajeshi na makundi ya waasi hawahusiki kwenye shughuli hii katili. Maelfu ya watoto bado wanaendelea kuingizwa jeshini na serikali na pia makundi ya waasi kwenye maeneo yanayokumbwa na mizozo hata baada ya jitihada za kimataifa kukabiliana na suala hilo.

Warsha ya kujiunga kwa nchi hizo iliandaliwa na shirika la kuwahudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF , afisi ya mwakilishi wa katibu mkuu wa UM kuhusu masuala ya watoto na mizozo na taifa la Ufaransa.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter