Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hispania kuisaidia Somalia kubadili maharamia kuwa wavuvi

Hispania kuisaidia Somalia kubadili maharamia kuwa wavuvi

Waziri wa mambo ya nje wa Hispania Miguel Angel Moratonis amesema, nchi yake itaisaidia Somalia kuimarisha sekta yake ya uvuvi katika juhudi za kupambana na uharamia uliokithiri pwani ya taifa hilo.

Akizungumza kwenye mkutano wa kundi la kimataifa liitwalo International Contact Group ICJ kuhusu Somalia uliomalizika jana mjini Madrid bwana Motratinos amesema lengo kuu ni kuwabadili maharamia wa Kisomali kuwa wavuvi. Jason Nyakundi na maelezo zaidi.

(RIPOTI YA JAYSON NYAKUNDI)

Akiongea na waandishi wa habari mjini Madrid wakati wa kumalizika kwa mkutano wa kundi la kimataifa liitwalo International Contact Gropu ICJ kuhusu Somali Moratinos amesema kuwa lengo kuu ni kuwabadili maharamia kuwa wavuvi. Morationos amesema kuwa uwezo nchi yake iliyo nao wa kutoa mafunzo ya uvuvi unaweza kusaidia serikali ya Somalia kutambua miradi ya kuijenga sekta ya uvuvi ya nchi hiyo.

Maeneo ya habari yanayoizunguka Somali yamekuwa ngome ya maharamia na kufanya shughuli za habarini kwenye maeneo hayo zilizo nyingi kuwa hatarini zaidi. Makundi ya maharanmia yamekuwa yakiendesha shughui zao kutoka kwa miji iliyo kando mwa pwani ya Somali na mara nyingi yameitisha fidia ya saidi ya dola milioni tano.

Meli kubwa za uvuvi kutoka Korea Kusini ,Japan na Uhispania zimekuwa zikiendesha uvuvi kiharamu kwenye eneo la bahari ya Somali tangu nchi hiyo kutumbukia kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 1991. Wengi wa maharamia hao wamedai kuwa awali walikuwa wavuvi waliolazimima kuacha uvuvi baada ya kupata ushindani mkali kutoka kwa wavuvi walio na vifaa vya hali ya juu kutoka nchi za nga'mbo.