Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uzalishaji maziwa utasaidia kupunguza umasikini:FAO

Uzalishaji maziwa utasaidia kupunguza umasikini:FAO

Ripoti mpya ya shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO imetoa wito wa fursa zaidi kwa usalishaji mdogo mdogo wa maziwa katika juhudi za kupunguza umasikini, kuinua kiwango cha lishe na kuboresha maisha ya watu wa vijijini katika nchi nyingi zinazoendelea.

Mkurugenzi wa FAO kitengo cha uzalishaji wa mifugo na afya Samuel Jutzi amesema mahitaji ya kimataifa ya maziwa yameongezeka kwa tani milioni 15 kwa mwaka hasa katika nchi zilizoendelea. Amesema endapo uzalishaji wa maziwa utaongezeka kutoka kwa wakulima wadogowadogo utatoa nafasi za kazi milioni 3 kila mwaka na hiyo kuchangia pakubwa katika kufikia malengo ya maendeleo ya milenia hususan kupunguza umasikini.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo iliyochapishwa leo kwa ushirikiano wa FAo na mtandao wa kimataifa wa ulinganifu wa mashamba IFCN kuna familia takribani milioni 150 au watu milioni 750 wanaojihusisha na uzalishaji mdogo wa bidhaa zitokanazo na maziwa na wengi wao ni kutoka katika nchi zinazoendelea.