Skip to main content

Uandikishaji kura ya maoni kuchelewa Sudan

Uandikishaji kura ya maoni kuchelewa Sudan

Serikali ya Sudan leo imetangaza kuchelewesha uandikishaji wa kura ya maoni nchini humo kwa muda wa wiki tatu.

Serikali inasema hata hivyo bado ina imani kwamba kurua hiyo itafanyika tarehe 9 Januari kama ilivyopangwa. Mamilioni ya wananchi wa Sudan wanatarajiwa kufanya maamuzi muhimu ya hatima ya nchi yao kwa kupiga kura kuamua endapo Sudan Kusini ijitenge na kuwa taifa huru ama la.

Taarifa kutoka kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa hapa New York zinasema ujumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa unatarajiwa kuzuru Sudan wiki ijayo ili kutoa shinikizo kwa viongozi wa Kaskazini na Kusini mwa nchi hiyo kuharakisha maandalizi ya kura hiyo ya maoni.

Wiki jana kwa kutambua umuhimu wa kura hiyo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki-moon aliteuwa watu watatu watakaofuatilia na kuangalia kwa makini kura hiyo ya mani. Ujumbe huo unaongozwa na aliyekuwa Rais wa Tanzania Benjamin William Mkapa.