Skip to main content

Kura ya maoni Sudan ni muhimu, na la msingi ni kukubali matokeo:Mkapa

Kura ya maoni Sudan ni muhimu, na la msingi ni kukubali matokeo:Mkapa

Kiongozi wa timu ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kuangalia kura ya maoni ya Sudan amesema jukumu lao kubwa ni kufuatilia hali na kutoa ushauri kwa wahusika.

Bwana Benjamin William Mkapa ambaye ni Rais wa zamani wa tanzania aliteuliwa wiki iliyopita na Katibu Mkuu Ban Ki-moon kuongoza timu ya watu watatu watakafualitia na kuangalia kura ya maoni ya Sudan Kusini. Mkapa amesema kura hiyo ni ya muhimu sana kwa hatma ya mamilioni ya Wasudan ambao watapiga kura Januari tisa kuamua endapo eneo la Sudan Kusini lijitenge na kuwa taifa huru ama la.

Bwana Mkapa akizungumza na mkuu wa Idhaa hii Flora Nducha amesema la msingi ni kwa watu kukubali matokeo mara kura hiyo itakapokamilika. Ungana nao katika mahojiano haya.