Japan imekuwa ya kwanza Asia kutoa makazi kwa wakimbizi

28 Septemba 2010

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema wakimbizi 18 leo wamewasili mjini Tokyo Japan ambako wataanza maisha mapya kama sehemu ya mpango wa kwanza kabisa barani Asia kutoa makazi kwa wakimbizi.

Wakimbizi hao ambao ni kutoka familia tatu na watoto wao 12 wenye umri wa kati ya mwaka mmoja hadi 15, ni wakulima kutoka jamii ya Karen ambao wamekuwa wakiishi kwenye kambi ya wakimbizi ya Mae La Kaskazini mwa Thailand tangu walipokimbia Myanmar.

Watoto karibu wote wamezaliwa walizaliwa kama wakimbizi Thailand. Wamewasili Japan kama sehemu ya mpango ambao Japan imekubali kupokea wakimbizi 90 wa Myanmar katika kipindi cha miaka mitatu na kuifanya nchi hiyo kuwa ya kwanza Asia kutoa makazi kwa wakimbizi.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter