Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Israel haikutoa ushirikiano:Tume ya flotilla

Israel haikutoa ushirikiano:Tume ya flotilla

Tume iliyoteuliwa na Rais wa baraza la haki za binadamu kuchunguza tukio la shambulio la meli ya flotilla Gaza Mai 31 jana imewasilisha ripoti yake kwa baraza hilo.

Mwenyekiti wa tume hiyo huru jaji K Hudson-Phillips ameliambia baraza la haki za binadamu kuwa serikali ya Israel haikutoa ushirikiano kwa tume hiyo. Amesema tume yao imebaini kuwa vitendo vya jeshi la Isarel na wafanyakazi wengine dhidi ya abiria waliokuwa kwenye meli ya flotilla havikustahili na kukiuka sheria.

Amesema majeshi ya usalama ya Israel yalitumia nguvu zisizohitajika na kusababisha vifo vya abiria 9 na kujeruhi wengine. Leo tume hiyo imekuwa na mkutano na waandishi wa habari mjini Geneva na haya ndiyo aliyosema mwenyekiti Hudson Phillips

(SAUTI YA K HUDSON PHILLIPS)