Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kukabili uharamia Somalia kunahitaji mshikamano:Mahiga

Kukabili uharamia Somalia kunahitaji mshikamano:Mahiga

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Dr Augustine Mahiga ameuambia mkutano wa ICG uliomalizika leo kwamba ili kumaliza tatizo la uharamia Pwani ya Somalia juhudi za pamoja zinahitajika.

Mahiga amesema nia ya jumuiya ya kimataifa inayoungwa mkono na serikali ya mpito ya Somalia lazima itekelezwe kama sehemu ya miakati ya hatua za kuleta utulivu wa kisiasa Somalia na sio kama mikakati binafsi.

Ameongeza kuwa ingawa shughuli za uharamia zimepungua kidogo kutokana na doroa inayofanywa na meli za kijeshi, kutoka 181 hadi 151 katika kipindi cha miezi 10 iliyopita lakini bado juhudi zinahitajika kutokomeza tatizo hilo. Amesema jumuiya ya kimataifa haijafanya juhudi za kutosha kushughulikia suala la uharamia.