Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Huduma kwa walioa na HIV na Ukimwi imeimarika katika nchi zinazoendelea:UM

Huduma kwa walioa na HIV na Ukimwi imeimarika katika nchi zinazoendelea:UM

Ripoti mpya iliyotolewa leo kuhusu masuala ya ukimwi inasema hatua kubwa zimepigwa katika nchi nyingi za kipato cha chini na cha wastani katika kupata huduma za masuala ya HIV na ukimwi.

Ripoti hiyo ambayo ni ya tathimini ya upatikanaji wa huduma kwa wote imeandaliwa na shirika la afya duniani WHO, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na shirika la Umoja wa Mataifa linalo husika na masuala ya Ukimwi UNAIDS, ni ripoti ya nne ya mwaka ya kufuatilia hatua zilizopigwa kufikia malengo ya 2010 ya kutoa fursa kwa wote kupata dawa za kuzuia, kutibu na kurefusha maisha kwa kwenye virusi vya HIV.

Ripoti hiyo imebaini kwamba nchi 15 zikiwemo Botswana, Guyana na Afrika ya Kusini zimefanikiwa kutoa zaidi ya asilimia 80 ya dawa kwa wanawake wajawazito na hasa katika kuzuia maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto. Na nchi 14 zikiwemo Brazili, Namibia na Ukraine zimetoa matibabu ya HIV kwa zaidi ya asilimia 80 kwa watoto.

Nazo nchi nane pamoja na Cambodia, Cuba na Rwanda zimefaulu kupata dawa za kurefusha maisha kwa watu wazima walioathirika na HIV. Dr Yves Souteyrand ni mratibu wa mipango na taarifa kwenye idara ya HIV na ukimwi wa WHO.

(SAUTI YA DR YVES SOUTEYRAND)