Skip to main content

Wakati umewadia Afrika tupate kiti kwenye Baraza la Usalama:Pinda

Wakati umewadia Afrika tupate kiti kwenye Baraza la Usalama:Pinda

Mjadala kwenye baraza kuu la Umoja wa Mataifa unaendelea huku viongozi na wawakilishi kutoka nchi zote wanachama wa Umoja wa Mataifa wakiwasilisha masuala wanayoona yanaisumbua dunia.

Mada mbalimbali zimeshajadiliwa ikiwemo utawala wa kimataifa, usalama na amani na leo tishio la ugaidi lilichukua nafasi kwenye Baraza la Usalama.

Waziri mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda ni miongoni mwa walihutubia mjadala huo leo, naye kaguzia masula hayo ikiwa ni pamoja na nia ya Afrika kutaka kiti cha kudumu kwenye Baraza la Usalama. Pinda anasema wakati umewadia na Flora Nducha akaketi naye chini na kumuuliza kwanini? sikiliza mahojiano haya.