Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Visiwa vidogo vinavyokua visaidiwe:Migoro

Visiwa vidogo vinavyokua visaidiwe:Migoro

Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Asha-Rose Migiro ameitaka jamii ya kimataifa kayapa usaidizi mataifa madogo ya visiwa yanayokua kwa sasa.

Bi Migiro amesema kuwa visiwa hivyo vimeathirika kiuchumi , kimazingiza na kwenye masuala ya kijamii kwa muda wa miaka kumi iliyopita hali inayosababisha visiwa hivyo kushindwa kutimiza melengo ya kimaendeleo ya kimataifa.

Akiguzia kati ya masuala yaliyojadiliwa kuhusu visiwa hivyo kando na mkutano mkuu wa umoja wa Umoja wa Mataifa Bi Migiro amesema kuwa athari zinazotoka nje zikiwemo hali mbaya ya uchumi duniani, ukosesu na kupanda kwa bei ya chakula na mafuta pamoja na mabadiliko ya hali ya hewa zimeongezea visiwa hivyo matatizo zaidi na hata kusababisha uwezekano wa kuendelea kuwepo kwa vingine kuwa mdogo zaidi.

 Mataifa madogo yananayokuwa kwenye visiwa yanakabiliwa na changamoto nyingi hasa kutokana na udogo wao , kutengwa , kutokuwepo na msingi dhabiti wa kuchumi na pia kuathirika zaidi na mabadiliko ya hali ya hewa duniani. Bi Migiro ameongeza kuwa juhudi zaidi zinahitajika kutekelezwa kwa ahadi za hapo awali za kuvisaidia visiwa hivyo.