Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake wapewe usalama kwenye maeneo ya mizozo:Ban

Wanawake wapewe usalama kwenye maeneo ya mizozo:Ban

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kufanya juhudi zaidi na kuwalinda wanawake na watoto wasichana kutokana na athari za kivita na kuhakikisha kuwa wameshirika vilivyo kwenye uzuiaji wa mizozo.

Akiongea mjini NewYork miaka kumi baada ya makubaliano ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu wajibu wa wanawake kwenye upatikanaji wa amani na usalama, Ban amesema kuwa huu ndio wakati wa kutekelezwa kwa makubaliono hayo.

Ban pia ametaka kusitishwa kwa dhuluma zinazotekelezwa dhidi ya wanawake na wasichana wakati wa mizozo na baada ya mizozo akisema kuwa wanawake ni lazima wawekwe kwenye msitari wa mbele wakati wa kutafutwa kwa amani. Ban pia ameongeza kuwa ni lazima kuwe na sheria mwafaka ili kuhakikisha kuwa wale wanaoendesha uovu dhidhi ya wanawake wamechukuliwa hatua za kisheria.