Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la haki za binadamu limepokea ripoti ya flotilla

Baraza la haki za binadamu limepokea ripoti ya flotilla

Tume huru ya kimataifa iliyoteuliwa na Rais wa baraza la haki za binadamu kuchunguza tukio la meli ya flotilla Gaza Mai 31 mwaka huu imewasilisha ripoti yake kwa baraza hilo.

Tume hiyo ambayo imewasilisha ripoti yake mjini Genenava inaongozwa na jaji K. Hudson Philips ambaye ni jaji wa zamani wa mahaka ya kimataifa ya uhalifu ya The Hague, na ina wajumbe wengine wawili Bwana Desmond de Silva aliyekuwa mwendesha mashitaka mkuu wa mahakama ya uhalifu ya Sierra Leone na Bi Shanthi Dairiam mtaalamu wa haki za binadamu wa Malaysia. Mwenyekiti wa tume ya wataalumu wa kufuatilia ripoti hiyo ni Christian Tomuschat.

(SAUTI CHRISTIAN TOMUSCHAT)

Tomuschat ameongeza kuwa kamati ina tumai na kuamini kwamba pande zote mbili zitaafiki matokeo ya ripoti ya yale yanayohitajika kushughulikia kutokana na uhalifu uliotendeka wakati wa shambulio la Gaza.