Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la usalama limesisitiza juhudi za pamoja katika kukabiliana na Ugaidi

Baraza la usalama limesisitiza juhudi za pamoja katika kukabiliana na Ugaidi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema ugaidi unaweza kuwa unaongezeka lakini juhudi za kimataifa za kukabiliana nao zinashika kasi.

Akizungumza kwenye baraza la usalama la Umoja wa Mataifa hii leo Ban amesema kuukabili ugaidi kunahitaji mtazamo mpana. Amesema ugaidi unatoa tishio kubwa la amani na usalama wa kimataifa.

Amesema nchi nyingi zinazoshiriki mkutano huo zina uzoefu wa athari za ugaidi kwa kushambulia na maisha ya watu wengi kupotea. Ban amekumbusha kwamba Umoja wa Mataifa pia umelengwa na ugaidi katika nchi kama Iraq, Pakistan, Algeria na Afghanistan

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

Katibu Mkuu ametoa wito wa kuendelea na juhudi za kupambana na ugaidi ikiwa ni pamoja na hatua za kuwanyika msaada wa fedha magaidi na uwezo wa kusafiri. Pia kuwazuia kupata na kutumia silaha za maangamizi.