Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM umejadili kura ya maoni Sudan na amani ya Darfur

UM umejadili kura ya maoni Sudan na amani ya Darfur

Kando na mjadala unaondelea kwenye baraza kuu la Umoja wa Mataifa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon jana usiku aliitisha mkutano maalumu wa kujadili suala la Sudan.

Mkutano huo uliohudhuriwa pia na makamu wa Rais wa Sudan Ali Osman Taha, makamu wa kwanza wa Rais wa Salva Kiir, Rais Baraka Obama, mwenyekiti wa muungano wa Afrika Jean Ping na viongozi wengine umejadili kura ya maoni ya Januari mwakani na suala la amani ya Darfur .

Akizungumza katika mkutano huo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema wakati wa kura ya maoni ni muhimu sana kwa taifa hilo.

(SAUTI BAN KI-MOON)