Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban apinga matumizi ya lugha na vitendo vinavyoleta mgawanyiko

Ban apinga matumizi ya lugha na vitendo vinavyoleta mgawanyiko

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo amezungumza kupinga matumizi ya lugha na vitendo ambavyo vinasababisha mgawanyiko na kutoaminiana miongoni mwa watu.

Akizungumza kwenye mkutano maalumu wa mawaziri wa ambao ni wa muungano wa ustaarabu kwenye baraza kuu la Umoja wa Mataifa hapa New York amesema dunia yeti imeungana zaidi lakini ina umoja mdogo. Kujenga imani ni jambo la muhimu sasa kuliko wakati mwingine wowote. Allince of Civilization ni mpango uliozinduliwa 2005 na Hispania na Uturuki chini ya chombo cha Umoja wa Mataifa chenye jukumu la kuchagiza mahusiano baiana ya tamaduni zote duniani.

Ameongeza kuwa mazungumzo ni muhimu sana hasa kwa masuala ya uchumi, kijamii na maendeleo ya binadamu. Amesema makundi madogo yanaweza kuleta maafa makubwa kwa vitendo vyao na matamshi yao na pia uwezekano wa machafuko kutokana tuu na lugha katika siasa na sehemu zingine za maisha.