Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afrika ya taka kura ya turufu kwenye baraza la usalama

Afrika ya taka kura ya turufu kwenye baraza la usalama

Viongozi wa Afrika leo wametoa wito kwa Umoja wa Mataifa kulipa bara hilo ujumbe wa kudumu kwenye baraza la usalama wakisema miaka 65 tangu kuanzishwa Umoja wa Mataifa bado umoja huo uko katika sera za zamani.

Akizungumza kwenye baraza la Umoja wa Mataifa Rais wa senegal Abdulaye Wade amesema kuhakikisha mnasalia kileleni kwa gharama yeyote inamaanisha ni kuyapa kisogo mabadiliko muhimu ya hali ya dunia na wakati huohuo kuliweka baraza katika hali ya kutoaminiwa zaid, kupingwa zaidi na kukosolewa zaidi.

Wade ameyasema hayo katika jitihada za kupigania kura ya turufu kwa bara la Afrika. Amesema toka wajumbe 51 mwaka 1945 hivi sasa Umoja wa Mataifa una wanachama 192, lakini bado baraza la usalama linalotakiwa kutoa matakwa ya pamoja, ambao maazimio yake ni kama kifungo limeongeza wajumbe mara moja tuu 1965 kutoka 11 hadi 15.

Wade ameuliza ni vipi mtu anaweza kuchukua jukumu muhimu la utawala wa kimataifa wakati Afrika ambayo ina zaidi ya robo ya vikosi vyake na inatawala asilimia 70 za ajenda za baraza la usalama haina ujumbe wa kudumu?