Skip to main content

Niger yautaka UM kuangalia chaguzi zinazofanyika nchini humo

Niger yautaka UM kuangalia chaguzi zinazofanyika nchini humo

Kiongozi wa Niger Salou Djibo ametoa wito kwa umoja wa Mataifa na mashirika mengine ya kimataifa kuangalia changuzi zinazotarajiwa kuandaliwa kwenye taifa hilo la Afrika Magharibi lililokumbwa na mzozo baada ya mapinduzi ya mwezi Februari mwaka huu.

Akihutubia baraza kuu la Umoja wa Mataifa Djibo amesema kuwa serikali ya mpito nchini Niger inataka kuona uchaguzi huru na wa haki ukifanyika. Mwezi Februari wanajeshi wa nchi hiyo walingia kwenye ikulu ya rais na kumuondoa mamlakani aliyekuiwa rias Mamadou Tandja ambaye alikuwa ameshutumiwa na upinzani kwa kwenda kinyume na masula ya kidemokrasia.

Uchaguzi nchini Niger unatarajiwa kuandaliwa kati ya tarehe 31 mwezi Oktoba mwaka huu na tarehe 6 mwezi Aprili mwaka 2011 ukianza na kupatikana kwa katiba mpya ambao utafuatia baadaye na wa kumchagua rais mpya ambaye ataapishwa tarehe 11 mwezi Aprili mwaka ujao.