Wachunguzi wa UM wathibitisha ubakaji wa watu wengi DRC

Wachunguzi wa UM wathibitisha ubakaji wa watu wengi DRC

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo leo Ijumaa imechapisha ripoti ya matokeo ya awali ya uchunguzi dhiti ya ubakaji wa kundi kubwa la watu na ukiukaji wa haki za binadamu uliotekelezwa na makundi ya watu wenye silaha kwenye mkoa wa Walikale kati ya Julai 30 na Agosti pili mwaka huu.

Jopo la wachunguzi wa Umoja wa Mataifa walizuru vijiji 13 vilivyoathirika katika eneo la Kibua-Mpofi mkoani Walikale kuendesha uchunguzi wa kina kuhusu dhuluma hiyo ya ubakaji na ukiukaji mwingine wa haki za binadamu.

 Matokeo ya awali ya uchunguzi huo yalitowekwa kwenye ripoti maalumu hii leo yanathibitisha kwamba watu zaidi ya 300 walibakwa wanawake, wanaume na watoto wa kike na wakiume pia. Msemaji wa shirika la haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Rupert Colville anafafanua.

(SAUTI YA RUPERT COLVILE)

Na wakati wa uhalifu huo nyumba 923 na maduka 42 yaliporwa na watu 116 walitekwa ili kufanyishwa kazi kwa nguvu.