Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bila msaada wa WFP nisingekuwa hapa nilipo leo: Paul Tergat

Bila msaada wa WFP nisingekuwa hapa nilipo leo: Paul Tergat

Paul Tergat mkimbiaji wa kimataifa kutoka nchini Kenya anasema biala WFP labda hata miguu yake isingeweza kukimbia au kuwa mwana riadha maarufu duniani.

Mwaka 1977 akiwa shule ya msingi nchini Kenya kupata mlo wa siku ilikuwa dhiki nyumbani kwao na mardi wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula WFP likawa mkombozi kwani lilianzisha mpango wa kuwalisha watoto shuleni kwenye jimbo la Rift Valley na kumuwezesha ketembea mili tatu kila siku kwenda shule.

Tergat ambaye sasa ana umri wa miaka 41, mke na watoto wane aliteuliwa kuwa balozi mwema wa WFP katika vita dhidi ya njaa 2004. Ameshawahi kushinda medali za fedha mbili za mashindano ya olimpiki, na kuvunja rekodi ya kuwa mshindi mara tano wa mbio za nyika za dunia, pia amewahi kujiandikia rekodi katika mbio za marathon.

Ni mmoja wa wakimbiaji bora wa mbio ndefu duniani. Kwa miaka sita sasa amekuwa akizunguka duniani kusaidia juhudi za WFP kuwalisha walio na njaa. Ameketi na Flora Nducha na kumuelezea safari ya maisha yake, wasikilize.