UNEP yajiunga kupunguza vifo vitokanavyo na majiko ya mkaa

23 Septemba 2010

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na mazingira UNEP limejiunga na mpango wa kimataifa wa kupunguza vifo na uharibifu wa mazingira vinavyosababishwa na majiko ya mkaa ya kupikia.

Watu wapatao bilioni 3 katika nchi zinazoendelea wanatumia majiko ya mkaa wakati wa kupika. Kwa mujibu wa UNEP moshi utokanao na kupikia ndani kwa majiko hayo unasababisha vifo milioni 1.8 kila mwaka na wengi wanaokufa ni wanawake. Majiko hayo pia yanaharibu mazingira. Mahitaji ya mkaa ni chanzo kikubwa na ukataji miti, mkaa pia unatoa gesi iitwayo black cabon na huenda inachangia asilimia 40 ya mabadiliko ya hali ya hewa hivi sasa.

UNEP inasaidia mradi wa kutengeneza majiko mazuri yanayojali mazingira nchini Ghana na ni majiko yanayotumia mkaa kidogo. Majiko 50,000 yameshatengenezwa hadi sasa na kutoa ajira kwa watu 200. Muungano wa kimataifa kwa ajili ya majiko bora ya kupikia una lengo la kugawa majiko milioni 100 katika kipindi cha miaka 10 ijayo.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter