Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Gabon yapongezwa kupinga ulanguzi wa binadamu na silaha

Gabon yapongezwa kupinga ulanguzi wa binadamu na silaha

Katibu mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalopambana na uhalifu (UNODC) amelipongeza taifa la Gabon kwa kutia sahihi makubaliano mawili yenye lengo la kukabiliana na ulanguzi wa binadamu na silaha akisema kuwa hatua hiyo itasaidia kuimarisha usalama na keleta amani katika eneo la afrika ya kati.

Yury Fedotov amesema kuwa ulanguzi wa silaha katika eneo la afrika ya kati umechochea mizozo zaidi inayotishia kuwepo kwa amani na kuchangia kuongezeka kwa dhuluma dhidi ya wanawake na pia kuingizwa kwa watoto jeshini. Amesema kuwa bila ya amani na usalama hakutakuwepo na maendeleo akiongeza kuwa hatua za haraka zinastahili kuchukuliwa ili kukabiliana na tatizo hilo.

 Kati ya makubalianio yaliyotiwa sahihi na Gabon ni pamoja kuwachukulia natua wale wanaohusika kwenye ulanguzi wa watu hasa kwa akina mama na watoto na yale ya kuzuia kuundwa kwa silaha haramu na ulanguzi wake. Makubalino yote mawili ni miongoni mwa mengine yanayotetea haki za binadamu yakiwemo ya utunzi wa mazingira, ya kutwaliwa kwa silaha, mabadiliko ya hali ya hewa, ugaidi na mengine mengi yanayoweza kutiwa sahihi