Skip to main content

Afrika yaahidi kukomesha vifo vitokanavyo na malaria

Afrika yaahidi kukomesha vifo vitokanavyo na malaria

Viongozi kutoka nchi za afrika na wataalamu wa afya kutoka sehemu mbali mbali duniani wameahidi kushirikiana kuupiga vita ugonjwa wa malaria na kuangamiza itimiapo mwaka 2015.

Kwenye mkutano uliofanyika baada ya kukalizika kwa mkutano mkuu wa umoja wa mataifa kuhusu malengo ya milenia, na kupitia kwa ujumbe uliowasilishwa na mjumbe wake maalumu kuhusu ugonjwa wa malaria Ray Chambers, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amesema kuwa hatua zimepigwa kwenye miaka ya hivi karibuni katika kupunguza vifo vinavyosababishwa na ugonjwa wa malaria na kwemye matumizi ya vyandarua vinavyozuia mbu.

Warsha hiyo iliyoandaliwa keenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa iliwaleta pamoja wanachama wa muungano inaopambana na ugonjwa malaria barani afrika ambao ni unawajumuisha viongozi 35 kutoka afrika walio na nia ya kushirikiana kuangamiza ugonjwa wa malaria barani afrika ambapo inakadiriwa kuwa unasababisha vifo vya zaidi ya watu 850,000 kila mwaka.

Kwenye mkutano huo viongozi wa afrika walitangaza kuchukua hatua kadha zitakazosaidia kupambana na ugonjwa huo zikiwemo za kuziondolea ushuru bidhaa zinazotumika kupambana na malaria yakiwemo madawa.