Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Madagascar yakataa kuhutubia mkutano wa malengo ya milenia

Madagascar yakataa kuhutubia mkutano wa malengo ya milenia

Wakati Rais wa Baraza la Umoja wa Mataifa Joseph Deiss akitambua hatua zilizoaninishwa na Madagascar ili kuyafikia malengo ya milenia, lakini viongozi wa Afrika wametia ngumu kuizua nchi hiyo isipewa nafasi kuhutubia mkutano huo uliokuwa ukiangazia hatua zilizopigwa kuyafikia mallengo hayo.

Mkutano huo wa siku tatu wa kutathmini namna nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa zinavyotekeleza malengo yake, ulimalizika jana usiku. Rais Joseph wakati akihitimisha mkutano huo alisema kwamba, kwa kuzingatia hali ya mazingira ilivyo sasa, Madagascar iliamua kutozungumza kwenye mjadala huo lakini hata hivyo akaipongeza namna ilivyomaanisha ili kuyafikia malengo hayo.

Rais wa Baraza la Umoja wa Mataifa amesema kuwa viongozi wa dunia wamekubali kuongeza juhudi ili kufikia shabaya iliyowekwa ya mwaka 2015 kwa malengo hayo yawe yamefanikiwa. Aidha alizipongeza nchi za Afrika kwa kubainisha vipaumbele vyao kukabiliana na matatizo kama njaa na umaskini.