Skip to main content

Mkutano wa kimataifa wa sekta ya posta umeanza Kenya

Mkutano wa kimataifa wa sekta ya posta umeanza Kenya

Zaidi ya wajumbe 550 kutoka nchi 16 duniani wanaowasilisha sekta ya posta wanakutana kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa ya mjini Nairobi Kenya kujadili hali ya sasa nay a baadaye ya sekta ya Posta.

Mkutano huo wa siku mbili ulioanza leo wa mikakati ya jumuiya ya kimataifa ya posta 2010 umefunguliwa na makamu wa Rais wa Kenya Kalonzo Musyoka na ni mara ya kwanza unafanyika barani Afrika. Wanaohudhuria mkutano huo ni pamoja na wawakilishi wa serikali, sekta za umma za posta, sekta binafsi, wafuatiliaji wa masuala ya posta, mashirika ya kimataifa na mashirika ya Umoja wa Mataifa.

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na huduma za posta Dayan amesema mkutano huo ni fursa kuangalia masuala yanayoathiri sekta ya posta wakati huu, ikiwepo teknolojia, huduma ya wateja, masuala ya uchumi na kifedha na utandawazi, na kasha kujadili njia za kuboresha sekta hiyo.