Kupungua msaada elimu kunatishia malengo ya milenia

23 Septemba 2010

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya elimu Kishore Singh ameonya kuwa kupungua kwa msaada katika sekta ya elimu kutaweka mashakani malengo ya maendeleo ya milenia.

Amesema matumizi ya serikali nyingi na msaada wa kimataifa kwa ajili ya elimu vimepungua kutokana na matatizo ya uchumi yaliyoikumba dunia hivi karibuni na hivyo kutishia hatua kubwa iliyopigwa katika kupata elimu ya msingi tangu kuanza kwa milenia.

Hata hivyo amesema hatua hiyi bado inawaacha watoto milioni 69 bila kuhudhuria shule jambo ambalo halikubaliki na linatakiwa kushughulikiwa. Akizungumza kwenye mjadala wa jukumu la elimu katika malengo ya milenia mjini New York bwana Sigh amesema msaada wa fedha kwa ajili ya elimu utakuwa na athari kubwa kwa nchi masikini.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter