Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Saratani ni changamoto kubwa Afrika:Mubarak

Saratani ni changamoto kubwa Afrika:Mubarak

Wataalamu wa saratani kutoka kote duniani wanakutana mjini Vienna Austria wiki hii kujadili ongezeko la matatizo ya saratani katika nchi zinazoendelea.

Katika mkutano huo wa siku mbili ulioandaliwa na shirika la kimataifa la nguvu za atomic IAEA unawaleta pamoja pia wawakilishi kutoka serikali mbalimbali, wataalamu wa afya na mashirika ya utafiti wa saratani.

Matatizo ya saratani yanaongezeka duniani na sasa ni chanzo cha vifio milioni 8 kila mwaka ,ikiwa ni idadi kubwa kuliyo ya ukimwi, kifua kikuu na malaria kwa pamoja, na asilimia 70 ya vifo hivi vinatokea katika nchi zinazoendelea.

Mke wa Rais wa Misri Bi Suzane Mubarak ni miongoni mwa waliozungumza kwenye mkutano huo na anaunga mkono vita dhidi ya saratani na nchi yake inasaidia nchi za Afrika kukabiliana na saratani

(SAUTI SUZANE MUBARAK)