Gabon, Malawi na Iran zasaini mkataba kutojumuisha watoto jeshini

22 Septemba 2010

Gabon, Jamhuri ya kiislamu ya Iran na Malawi zimekuwa nchi za hivi punde kutia sahihi makubaliano ya kulinda haki ya watoto kwa kutowatumia watoto kama wanajeshi hasa wakati wa mizozo kwenye hafla uliyofanyika sambamba na mkutano wa mwaka huu wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa.

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon kwenye masuala ya watoto na mizozo Radhika Coomaraswamy amewashukuru mawaziri walioshirikia hafla hiyo kwa hatua waliyochukua. Amesema kuwa makubaliano hayo yatahakikisha kuwa hakuna mtoto ambaye atalazimishwa kupigana vita wala kuingia jeshini.

Hata hivyo bado makubaliono hayo hayajatiwa sahihi na wanachama wengine zaidi ya 50 huku wanachama saba wakiwa tayari wameyatia sahihi makubaliano hayo tangu kuanza kwa kampeni hiyo mwezi mei mwaka huu. Ameongeza kuwa kujiunga hawatatumika vitani bali watapewa haki ya kukua kama watoto.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter