Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sekta ya chakula Haiti imeanza kuimarika japo uzalishaji mdogo:UM

Sekta ya chakula Haiti imeanza kuimarika japo uzalishaji mdogo:UM

Tathimini ya pamoja ya mashirika mawili ya Umoja wa Mataiifa imebaini kwamba sekta ya chakula nchini Haiti inaanza kuimarika lakini uzalishaji bado mdogo ikilinganishwa na kabla ya tetemeko.

Shirika la mpango wa chakula WFP na shirika la chakula na kilimo FAO yanasema licha ya uharibifu uliokumba mfumo wa uzalishaji wa chakula nchini Haiti kutokana na tetemeko la Januari, mvua zinazonyesha sasa zimesaidia kufufua kilimo nchini humo.

FAO na WFP ambao walikuwa wanafanya tathimini ya mazao na usalama wa chakula Haiti tangu Juni 16 hadi Julai 13 mwaka huu wamebaini kwamba mavuno ya mwaka huu hasa ya mahidi, uwele na ndizi yameshuka kwa asilimia 17 ilikilinganishwa na mwaka 2009.