Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kujiuzuru kwa waziri mkuu Somalia ni ishara ya mgawanyiko:UM

Kujiuzuru kwa waziri mkuu Somalia ni ishara ya mgawanyiko:UM

Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Dr Augustine Mahiga amesema ametambua uamuzi wa waziri mkuu wa Somalia Omar Abdirashid Sharmarke kujiuzulu kwa masilahi ya amani na usalama nchini humo.

Amesema hata hivyo kujiuzulu kwa bwana Sharmarke ni ishara nyingine ya mgawanyiko mkubwa ulioko katika serikali ya mpito ya Somalia na ni matumaini yake kwamba serikali hiyo ya mpito sasa itamaliza mgawanyiko uliopo ambao umeilemaza zaidi serikali hiyo katika kutekeleza majukumu yake. Mahiga amesema serikali ya mpito ni lazima iwe na mshikamano na kuzingatia majukumu yake.

Amesema ni chini ya mwaka mmoja kabla ya serikali hiyo kumaliza muda wake hapo Agosti 2011 na kuna kazi kubwa inayohitaji kukamilishwa . Amezitaka pande zote zinazopenda amani kushirikiana kufanya kazi pamoja kwa maslahi ya nchi ya Somalia na watu wake.